Pata copy yako

KATIKA kile kinachoonekana kuwa ni mapinduzi ya sanaa ya uchoraji katuni nchini, Msanii mkongwe katika fani hiyo ambaye mimi namheshimu sana, David Chikoko kwa kushirikiana na Frederick Gerniers kutoka Belgium wanakuletea comic story book ya Tom & Jenny nchini Tanzania… Advertisements

Nakala ziko chache!

KWA kununua products zetu mna support kukuza sanaa na wasanii wa nyumbani, Kitabu hicho pamoja na T-shirts za babatau vinapatikana sehemu mbalimbali lakini pia unaweza kupata kutoka kwa babatau moja kwa moja kupitia namba 0713 474 200 nasi tutakufikia!!!

kuelekea uchaguzi 2010

Tunapoelekea uchaguzi kuna kero nyingi zinatuzunguka katika maisha yetu, kama mdau wa katuni Hebu fikiria maneno yanayoweza kufikisha ujumbe kwenye katuni hii! kisha tuandikie jina lako na unapotoka, tutauchapisha ili uwafikie walengwa!

kuelekea uchaguzi mkuu!

KWA jicho la tatu tutakuwa tukikuonesha hali halisi ya maisha yetu kuelekea uchaguzi mkuu kisha we mwenyewe utapambanua na kutuandikia maoni yako! Katuni hii inakuonesha jinsi serikali inavyopata fedha ili kupambana na umaskini! we unaona nini?

uhasama barabarani!

Fikiria maneno unayoona yanafaa kwenye hii katuni ili ikamilike, kisha tutumie jina lako na mahali unapotoka! Jaribu kufupisha maneno yasiwe mareeefu lakini yalete maana! Natumai wadau mnanielewa!

nyumba ya gavana wa BoT!

Unafikiri hawa wananchi wanasemaje kuhusu hili? tuandikie chini maoni yako!

Ufisad!

Nashukuru sana wadau mliojitokeza kujaza maneno ya kumalizia hii katuni,  nimefurahi kwamba tuko pamoja  na mawazo yenu nayafanyia kazi! Napenda nimpongeze ndugu ROBSON BANZI hajasema anatokea wapi lakini huyu ndo kafanikiwa kubuni maneno hayo yaliopo kwenye katuni: “OOH NO SASA TOO MUCH HATA HII WAMEIGUNDUA!! WATANIUA SOON HAWA”

Bado nakumbuka!

NILIPORUDI  vekesheni nikakuta Taifa lipo katika simanzi kuu ya kupotelewa na Mzee wetu Simba wa vita Rashid Kawawa, Ilikuwa ni habari iliyotia simanzi lakini habari nyingine iliyonistua ni baada ya kusikia taarifa za kifo cha Mzee Vumi Urassa, aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya The Guardian, Taarifa hizi zilinikumbusha vifo vya wazazi wangu pale nilipompoteza … Continue reading

Vacation!

Nilikuwa vekesheni ya muda toka mwezi Oktoba mwaka jana lakini sasa nimerudi na mambo makubwa katika ulimwengu wa katuni hivyo wadau stay TOOOOOOONED!!!! hapahapa! (Picha hii kwa hisani ya Muhidin Issa Michuzi)